DCSIMG
Skip Global Navigation to Main Content
Texts & Transcripts

State’s Carson at Wilson Center on U.S.-Africa Partnership (Kiswahili)

18 January 2013

Ushirikiano wa Marekani na Afrika: Miaka Minne Iliyopita na Zaidi
Katibu Msaidizi Carson
The Wilson Center, Washington
Kama Ilivyotayarishwa kwa Kuwasilisha

Asante. Nataka kumshukuru Michael kwa hotuba yake ya ufunguzi, na Michael na Steve kwa kunipokea hapa leo. Nataka pia kuwashukuru wageni wote wa heshima waliohudhuria , pamoja na wanachama wa ubalozi na wenzetutoka jamii ya think tank. Ni heshima kuzungumza na kundi lenye taadhima kama hilo la viongozi ambao, kama mimi, wamejitolea kusaidia bara la Afrika . Namshukuru pia mke wangu, Anne. mimi na yeye tumetumia muda wetu mwingi katika maisha yetu tukifanya kazi katika bara la Afrika, na hakuna kitu chochote nilichokamilisha kingekuwa kimewezekana bila ushauri wake, ushirikiano, na msaada.

Shauku yangu ya bara la Afrika ilianza ilianza katikati ya 1960 wakati nikihudumia Jamii ya Amani nchini Tanzania. Miaka ya 1960 ilikuwa ni wakati wa ahadi kubwa kwa Afrika. Mataifa mapya huru yalijitahidi kukabiliana na kile wengi walichoona kama changamoto isiyoweza kuondolewa ya demokrasia, maendeleo na ukuaji wa uchumi, watu waliokuwa wamepata uhuru mpya walitarajia kukubali enzi za fursa na matumaini. Ahadi hii pia ilinihamasisha kuingia kwenye Huduma ya Kigeni. Baada ya zaidi ya miaka arobaini ya ujuzi katika Afrika, balozi mara tatu, na sasa miaka minne kama Katibu Msaidizi wa Maswala ya Afrika, nimejionea ushindi wa hali ya juu, misiba, na maendeleo ya Afrika. Na licha ya kiwango cha maendeleo Afrika kutofautiana, ninaendelea kuwa na matumaini makubwa kuhusu mustakabali wa Afrika. Matumaini haya ni msingi katika upanuzi wa demokrasia, uboreshaji wa usalama, ukuaji haraka wa uchumi, na nafasi kubwa zaidi kwa watu wa Afrika. Ni wazi kwamba karne ya 21 haitaundwa tu Beijing na Washington, lakini pia Pretoria na Abuja.

Napenda kuanza leo kwa kuangazia maeneo mawili ambapo hakuna mtu aliamini matumaini yale yangewezekana: Somalia na Sudan Kusini.

Mkakati wa Rais Obama na Waziri Clinton kwa ajili ya Somalia umegeuza moja ya migogoro ya Afrika iliyodumu zaidi, kaidi, na inayoonekana kutokuwa na matumaini katika hadithi ya mafanikio makubwa na mfano unaowezekana wa kutatua migogoro mingine katika bara. Tangu kuanguka kwa serikali ya Siad Barre katika mwaka 1991, zaidi ya watu milioni moja wameuawa nchini Somalia. Marekani na washirika wengine wa kimataifa kwa kiasi kikubwa waliiwachilia Somalia kufuatia mkasa wa Black Hawk Down mwaka wa 1993. Somalia ilitoa kambi ya wakimbizi kwa baadhi ya magaidi ambao waliangamiza Ubalozi wetu mjini Nairobi mwaka 1998, na vile vile kuua Wamarekani na Wakenya kwa pamoja, na ambao walijaribu bila mafanikio kufanya hivyo hivyo jijini Dar es Salaam. Mapema katika Utawala huu, Waziri Clinton na mimi tulisafiri kwenda Nairobi kukutana na Sheikh Sharif, aliyekuwa rais wa Serikali ya Mpito ya Shirikisho ya Somalia wakati huo, au TFG. Sharif hapo awali aliwahi kuwa Mkuu wa Umoja wa Somalia wa Mahakama za Kiislamu, na hatukuwa na uhakika wa uwezo wake wa kupambana na makundi ya kigaidi kama al Shabaab au kuongoza demokrasia ya mpito ya Somalia.

Baada ya mkutano na Rais Sharif, Waziri Clinton aliniambia mambo mawili: "Usiruhusu kuanguka kwa TFG" na "Usiruhusu kushinda kwa al Shabaab." Naam, kama nyote mnavyoweza kufikiria pengine, sikuweza kupata usingizi usiku kufuatia majadiliano yale. Lakini tangu wakati huo, Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ilishirikiana na Tume ya Umoja wa Afrika nchini Somalia, au AMISOM, kutoamafunzo kwa majeshi ya kulinda amani kutoka Uganda, Burundi, Djibouti, na sasa Kenya na Sierra Leone kujenga upya Jeshi la Taifa la Somalia na kushinda al Qaida na al Shabaab . Marekani pia ilijiunga na washirika wa Afrika Mashariki ili kuendeleza njia ya kisiasa ambayo, katika mwaka wa 2012, iliwezesha Rais Sharif na TFG kumkabidhi mamlaka Rais wa Somalia aliyechaguliwa kidemokrasia.

Juhudi hii iliongozwa na waafrika, lakini ilipata msaada mkubwa toka Marekani. Mafanikio yake ni ya ajabu. Miaka minne tu iliyopita, al Shabaab ilidhibiti upande mkubwa zaidi wa Mogadishu na kusini na katikati mwa Somalia. Leo, AMISOM na Vikosi vya Usalama wa Taifa vya Somalia kuwa waliondoa al Shabaab kutoka Mogadishu na kila mji mwingine mkubwa nchini Somalia. Sasa, kwa mara ya kwanza katika zaidi ya miongo miwili, Somalia ina serikali wakilishi na Rais mpya, Bunge jipya, Waziri Mkuu mpya, na Katiba mpya, na watu wa Somalia wanayo sababu ya matumaini ya maisha bora ya siku za usoni. Mimi binafsi nilishuhudia mabadiliko haya mapya ya fursa na matumaini niliposafiri kuelekea Mogadishu Juni 2012, na kuwa Waziri Msaidizi wa kwanza kutembelea Mogadishu kwazaidi ya miaka 20. Marekani itaendelea kushirikiana na watu wa Somalia wanavyoendelea kujenga upya nchi yao na kurejesha mahusiano yao katika jimbo hili, na ninatazamia siku ambapo Marekani itweza kuanzisha tena uhusiano wa kidiplomasia wa kudumu zaidi Mogadishu, na kusaidia pakuu juhudi mpya za serikali ya Somalia za kutoa usalama, misaada ya kibinadamu, na huduma za msingi kwa wananchi wake.

Ufanisi mkubwa wa pili wa utawala huu ulikuwa kusaidia kupata amani ambao ulisababisha kuundwa kwa taifa jipya zaidi la Afrika: Sudan ya Kusini. Kuendeleza kazi ya utawala wa awali, Rais Obama aliendeleza jitihada za Marekani za kutekeleza kikamilifu Mkataba wa Amani Mpana wa Sudan, au CPA, na kumaliza vita vya wenyewe vilivyodumu zaidi katika Afrika. Chini ya uongozi wa Wajumbe Maalum wa Rais Obama, Scott Gration na kisha Princeton Lyman, Marekani iliongoza juhudi za kimataifa za kuimarisha CPA. Uongozi wa Rais Obama, Waziri Clinton, na Balozi Rice ulilainisha kura ya maoni ya Januari 2011 ya uhuru wa Sudan ya Kusini, na kusababisha kupata uhuru kwa Sudan ya Kusini miezi michache baadaye. Mjumbe Maalum Lyman anaendelea kufanya kazi pamoja na Sudan, Sudan ya Kusini, Umoja wa Afrika, na wengine wengi ili kuhakikisha amani na utulivu wa kudumu kati ya nchi hizo mbili.

Maendeleo haya ya ajabu nchini Somalia na Sudan ya Kusini yanaonyesha mafanikio ya ujumla ya sera ya Utawala huu kwa ajili ya bara la Afrika. Sera hii, inayoelezwa katika Mkakati wa Marekani kwa ajili ya Afrika ya Kusini mwa Sahara, ni pana. Inalenga ujenzi wa ushirikiano na serikali, jamii za kiraia, na idadi ya watu kote barani Afrika ili kuimarisha taasisi za kidemokrasia; kuchochea ukuaji wa uchumi, biashara, na uwekezaji; kuendeleza amani na usalama; na kukuza fursa na maendeleo.

Ushirikiano ni muhimu hasa kwa ajili ya kuendeleza nguzo ya kwanza ya mkakati huu: kuimarisha taasisi za kidemokrasia za Afrika, kuboresha utawala, na kukuza haki za binadamu. Kujitolea kwa demokrasia na haki za binadamu ni maadili ya pamoja ambayo yanaunganisha wananchi wa Marekani na idadi ya watu kote Afrika. Na lengo la Rais Obama na Waziri Clinton juu ya malengo hayo ya pamoja limekuwa na athari nzuri kote barani.

Nchini Naijeria, wakati Rais Yar Adua alipougua na kufariki, Marekani ilitoa mawazo bila kusita. Tuliwaunga mkonoWanaijeria ambao walisisitiza kwamba ni lazima katiba ya Naijeria ifuatwe na kwamba jeshi la Naijeria linapaswa kusalia kambini. Mimi binafsi nilisafiri hadi Naijeria ili kuwatia moyo viongozi wakuu wote wa miaka kumi iliyopita ili wafuate katiba, na kuwaomba kwamba pasiwe na jaribio hata moja la kuuteka nyara mchakato wa kisiasa. Baada ya mwanzo mbovu, uchaguzi wa Naijeria ulikwenda vizuri. Na wakati wa raundi ya kwanza ya uchaguzi wa 2011, nakumbuka nikiona wafanyakazi wa uchaguzi wa Kinaijeria waliokuwa wamejitolea wakihesabu kura za urais kwa kutumia tu mwanga kutoka kwenye simu zao za mkononi. Kujitolea kwa wafanyakazi vijana wa uchaguzi wa Nijeria, mamia ya maelfu ya Wanaijeria ambao walisubiri kwenye foleni kwa saa nyingi ili kupiga kura, na wale wote nchini Naijeria ambao walifanya kazi ili kuweka mchakato wa kisiasa wa Naijeria katika njia nzuri walihakikisha mafanikio ya uchaguzi wa mwaka 2011 na kuthibitisha fursa na matumaini mapya ya Afrika.

Nilishuhudia kujitolea huko kwa demokrasia nchini Kenya mwaka 2010. Marekani ilifanya kazi sambamba pamoja na Wakenya kote nchini ili kuhakikisha kura ya maoni ya katiba yenye amani iliyoundwa ili kupunguza wachochezi wa mgogoro wa kisiasa ambao uliwaua Wakenya wengi kufuatia upinzani dhidi ya uchaguzi wa mwaka 2007.

Ujumbe wetu kote Afrika kwa ambao wamejaribu kuzuia mchakato wa kidemokrasia umekuwa wazi: Marekani haitasimama pembeni wakati serikali zilizochaguliwa kihalali zinatishiwa au michakato ya kidemokrasia inachezewa. Wakati desturi za kidemokrasia za Senegal zilitishiwa, nilitoa mwito kwa Rais Abdoulaye Wade kutimiza kanuni zake za kidemokrasia na kulinda katiba ya Senegali. Alipochagua kuweka maslahi yake mwenyewe juu ya yale ya wananchi wake, tulienda kwa upande wa wananchi wa Senegali. Senegali hatimaye ilifanya uchaguzi mwingine wa amani, kidemokrasia na uhamisho wa mamlaka. Wakati halmashauri ya kijeshi nchini Guinea-Conakry ilifanya unyanyasaji mkubwa wa haki za binadamu, tulichukua hatua. Tukifanya kazi kwa pamoja na serikali za Moroko, Burkina Faso, na Ufaransa, Marekani ilikabili viongozi wa halmashauri ya utawala, na nilikutana binafsi na Jenerali Konate mjini Rabat. Diplomasia yetu ilitoa njia ya uchaguzi huru,wa haki, na wa amani wa kwanza wa Guinea, , tangu kupata uhuru mwaka 1958. Wakati mapinduzi ya kijeshi yalitokea nchini Naja na Mauritania, tulifanya kazi na viongozi wa ndani, washirika wa kieneo, na jumuiya ya kimataifa ili kurejesha demokrasia katika nchi zote mbili kwa haraka iwezekanavyo. Na katika Cote d'Ivoire, wakati Rais Gbagbo alipuuza matokeo ya uchaguzi wa nchi yake, Rais Obama alijaribu kuwasiliana na Gbagbo, mara mbili, ili kumhimiza ajiuzulu. Wakati hali iliendelea kuwa ya kutostahimilika nchini Cote d'Ivoire, tulihimiza Umoja wa Mataifa kuchukua hatua. Gbagbo yupo sasa katika Mahakama ya Hague, na demokrasia imerudishwa mjini Abidjan.

Bila shaka, demokrasia na haki za binadamu ni muhimu zaidi ya kufanya uchaguzi. Kama Rais Obama alivyosema nchini Ghana mwaka 2009, "Afrika haina haja ya watu wenye nguvu, inahitaji taasisi imara." Hii ina maana kuwa mahakama huru, mabunge, na tume za uchaguzi. Ina maana vyombo huru vya habari, utawala wa sheria, na mashirika ya kiraia ya ndani yaliyo na nafasi ya kuendesha kazi na kuongea kwa uhuru bila vitisho kutoka kwa mamlaka ya serikali. Na ina maana kuheshimu uwezo wa vyama vya upinzani wa kushiriki katika maandamano ya amani ya umma na kuwapinga wale walio katika madaraka kwa uwazi.

Kote barani Afrika, Rais Obama, Waziri Clinton, nami tumefanya kazi kwa kuimarisha uwezo wa wabunge kutekeleza majukumu ya usimamizi na ufanisi zaidi. Tulishirikiana pamoja na vyombo vya habari barani Afrika na mashirika ya kiraia ili kukuza na kulinda uhuru wa vyombo vya habari. Tuliunga mkono mipango ya utawala wa sheria ya kuimarisha mahakama za Afrika na tume za kitaifa za haki za binadamu ambazo ni muhimu kwa ajili ya kuondoa hali ya kutokujali na kuhakikisha haki kwa watu wote, bila kujali jinsia, umri, kabila, dini, rangi, au mwelekeo wa kijinsia. Ili kutoa kipaumbele kwa umuhimu wa mahakama, msimu uliopita tuliwaalika Marekani majaji maarufu wa Kiafrika wa mahakama kuu ambapo walikuwa na fursa ya kukutana na Hakimu Mkuu Roberts na Majaji Kennedy na Ginsberg.

Nchini Sierra Leone, tuliunga mkono Mahakama Maalum iliyowajibika kumhukumu Charles Taylor nawatuhumiwa wengine waliosababisha ukatili wakati wa vita vya kikatili vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo. Na nchini Uganda, Waziri Clinton aliwasilisha Tuzo la Waziri la Mtetezi wa Haki za Binadamu la 2011, ambalo ni tuzo la kimataifa la kifahari zaidi la haki za binadamu katika Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje, kwa muungano wa MASHIRIKA YASIYO YA SERIKALI (NGOs) LGBT.

Ushirikiano wetu na Afrika juu ya demokrasia, utawala bora, na haki za binadamu ni muhimu mno, lakini ni eneo moja tu la ushirikiano wetu. Rais Obama, Waziri Clinton, nami pia tulitumia nguvu katika kukuza upanuzi wa uchumi wa Afrika.

Uchumi wa Afrika ni miongoni mwa ule unaokuaharaka katika sayari, na wanazidi kuvutia biashara ya nje na uwekezaji. Na mabadiliko ya kiteknolojia yanajitokeza kote Afrika. Leo, wanawake katika masoko ya vijijini nchini Naijeria wanatumia simu za mkononi ili kuhamisha fedha na kuangalia bei katika masoko kadhaa ya vijiji vilivyo mbali. Benki katika Dakar zinafanya biashara na Wachuuzi mjini New York. Haya ni mabadiliko, mapinduzi ya kusisimua. Kulingana na jarida la The Economist, saba kati ya uchumi kumi unaoongezeka kwa kasi ulimwenguni upo barani Afrika. Jambo moja ambalo takwimu hii inamaananisha ni kuwa Afrika inaanza kufikia uchumi wa dunia. Ukiangalia orodha ya nchi saba, kadhaa kati yazo, kama vile Zambia, Ghana, na Ethiopia, inazidi tata uchumi ambapo ukuaji wa pamoja na tabaka la kati limechukua umiliki. Ukuaji usiohusiana na mafuta una wastani wa asilimia tano barani Afrika katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, na zaidi ya miaka mitano ijayo wastani wa kiwango cha ukuaji wa Afrika unaweza kupita ule wa Asia.

Mielekeo hii inabadilisha daima mifumo ya uchumi na siasa ya Afrika kwa kuionyesha dunia. Hata hivyo sio wafanya biashara wakutosha wa Kimarekani wanajua kwamba kama unataka kufanya uwekezaji mzuri, unapaswa kuangalia bara la Afrika. Hii ndiyo sababu kwa kipindi cha miaka minne iliyopita, Utawala huu ulifanya kazi ya kupanua biashara ya Marekani na uwekezaji na bara la Afrika. Tuliongeza muda wa utoaji wa vitambaa wa nchi zinazoendelea wa Sheria ya Kiafrika ya Ukuaji na Fursa, au AGOA, ambayo imesaidia kuweka mamia ya maelfu ya ajira katika bara. Tulihudhuriavikao vya AGOA nchini Kenya, Zambia, Mji wa Kansas , na Cincinnati, tukiunganisha sehemu kubwa ya makampuni na wawekezaji wa Kimarekani pamoja na washirika wa Kiafrika. Misheni ya kibiashara ambayo Waziri Clinton aliongoza kuelekea Afrika Kusini katika Agosti mwaka jana ilikuwa misheni ya kwanza kabisa ya kibiashara ilioongozwa na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje barani Afrika. Misheni tofauti nilizongoza mwaka jana nchini Msumbiji, Tanzania, Naijeria, na Ghana ziliongeza maslahi ya makampuni ya nishati ya Marekani katika haja kubwa kwa ajili ya uzalishaji, usambazaji, na mgawanyo wa nguvu za umeme katika bara zima. Na mmoja wa washiriki katika misheni hii tayari amesaini mkataba na kampuni ya Naijeria ambayo inatarajiwa kuzalisha makumi ya mamilioni ya dola yenye thamani ya mauzo ya nje ya Marekani na kutoa umeme unaohitajika mno nchini Naijeria.

Tunawezesha pia wajumbe wa biashara zaidi na zaidi kutoka upande mwingine kutoka Afrika kuelekea Marekani. Mwezi uliopita tu, Balozi wetu nchini Naijeria aliongoza watendaji wa kibiashara wa Naijeria katika maonyesho makubwa ya kibiashara mjini New Orleans na Orlando. Na tangu 2009, Shirika la Marekani la Uwekezaji wa Kibinafsi, au OPIC, liliunga mkono uwekezaji wa sekta binafsi yenye jumla ya zaidi ya dola bilioni 2 katika Afrika - rekodi ya muda wote - na kufungua ofisi mpya katika Afrika Kusini ili kukuza miradi midogo midogo ya ya nishati..

Na tuliendelea kujijenga juu ya kazi hii yote. Mwezi wa Novemba, Kaimu Waziri wa Biashara Blank alitembelea eneo hilo - mara ya kwanza Waziri wa Biashara wa Marekani amesafiri katika Afrika ya Kusini mwa Sahara kwa zaidi ya muongo mmoja - na kutangaza uzinduzi wa Kufanya Biashara katika Kampeni ya Afrika. Kampeni hii inahimiza makampuni ya Marekani kuchukua fursa katika Afrika itafanya iwe rahisi kufanya hivyo.

Lakini kwa vile ukuaji wa demokrasia na uchumi huenda sambamba na usalama na utulivu, Utawala huu pia ulipanua ushirikiano unaolenga mafunzo kwa vikosi vya kulinda amani vya Kiafrika, kusaidia juhudi za Afrika za kuunda Nguvu Zilizo Tayari, na zinazokabiliana na vitisho vya kimataifa kama uharamia, dawa za kulevya, na ugaidi. Nilibainisha tayari mafanikio ya ajabu ya AMISOM kama mfano wa kuigwa kwa kuwa ni operesheni ya ulinzi wa amani inayoongozwa Afrika kulinda amani. Kwa kushirikiana na Uganda; Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, au DRC; Jamhuri ya Afrika ya Kati, Sudan ya Kusini; na Umoja wa Afrika, Marekani pia inaunga mkono juhudi za kuondoa vitisho vinavyotokana na Ukatili wa Lord's Resistance Army. Nchini Mali, Marekani inaunga mkono hatua za kijeshi za Kifaransa, kuharakisha kupelekwa kwa ECOWAS na utoaji wa misaada kwa Utume huo unaoongozwa na Afrika, haja ya mkakati wa kurejesha utawala wa kidemokrasia, na misaada ya haraka ya kushughulikia mahitaji ya kibinadamu.

Mashariki mwa DRC, ambako zaidi ya watu milioni tano wameuawa katika kipindi cha miaka 15 ya unyanyasaji, Marekani inafanya kazi pamoja na Umoja wa Mataifa, washirika wa Ulaya, na wa kieneo ili kutambua suluhu za haraka na za muda mrefu ili kumaliza kujirudia kwa ukosefu wa salam katika mashariki mwa Kongo. Katika Novemba 2012, wakati kikundi cha waasi M23 kilichukua udhibiti wa mji wa Goma, nilisafiri mjini Kampala, Kigali, Kinshasa pamoja na wenzangu wa Uingereza na Ufaransa ili kutoa ujumbe maalum kwa Uganda, Rwanda, na DRC. Baada ya misheni hii, M23 iliondoka, na Rais Kagame, Kabila, na Museveni walianzisha mazungumzo.

Nguzo ya nne ya Shughuli za Utawala huu pamoja na Afrika - ikiwa ni pamoja na demokrasia, usalama, na ukuaji wa uchumi - ni kukuza fursa na maendeleo, kwa kulenga hasa wanawake na vijana. Wanawake wanajumuisha nusu ya idadi ya watu barani Afrika, lakini mara nyingi hutengwa kushiriki katika uchumi rasmi wa Afrika. Ili kukabiliana na ukosefu huu wa kutosawazisha, tuliongeza jitihada za kidiplomasia na maendeleo yaliyoundwa kuwezesha wanawake na wasichana kupitia mipango kama Mpango wa Ujasirimali wa Wanawake wa Kiafrika. Na tulishirikiana na kizazi kijacho cha viongozi wa Afrika kupitia Mpango wa Rais wa Viongozi vijana wa Afrika. Rais na Mkewe waliandaa binafsi matukio nchini Marekani na Afrika yanayolenga kuendeleza na kusaidia viongozi chipukizi wa Afrika, kukuza ujasiriamali, na kujenga ushirikiano kati ya Waafrika na Wamarekani chipukizi.

Tuliona pia matokeo mazuri katika ajenda yetu ya maendeleo. Kupitia mpango wa Rais "Feed the Future", tulishirikiana na nchi kumi na tisa za Afrika ili kupunguza utapiamlo. Waziri pamoja nami tulikuwa na furaha ya kukutana na wakulima nchini Malawi ambao, kwa msaada wa Marekani, walichangia ongezeko la asilimia 500 katika uzalishaji wa maziwa katika muongo uliopita. Na Rais Obama alizindua Muungano Mpya ya Usalama wa Chakula na Lishe kupitia G8, ambao unalenga kutoa Waafrika milioni 50 kutoka katika umaskini kwa kipindi cha miaka kumi ijayo. Kupitia Mpango wa Rais wa Afya ya Kimataifa na Mpango wa Dharura kwa msaada wa UKIMWI, au PEPFAR, tuliunga mkono mageuzi ya mfumo wa afya na matibabu ya kuokoa maisha ambao ulisaidia maisha ya watu karibu milioni tano wenye ukimwi katika Afrika. Na kupitia Shirika letu la Changamoto za Milenia, au mikataba ya MCC, tumewekeza karibu dola bilioni 6 katika nchi kumi na nne za Afrika ambazo zimeonyesha kujitolea taasisi imara za kidemokrasia, uwajibikaji, na uwazi. Na Liberia, Sierra Leone, na Niger - nchi tatu ambazo hivi karibuni zilirejesha utawala wa kidemokrasia na kuibuka kwa kasi kama viongozi wa kieneo kwa upande wa maendeleo, uwazi, uwajibikaji, na ukuaji - hivi karibuni zilichaguliwa kama zinazostahili kuendeleza mikataba mipya ya MCC.

Msaada wa maendeleo wa Marekani pia umelenga katika kuboresha afya ya mama na mtoto, kupambana na malaria, na kuboresha upatikanaji wa elimu bora katika Afrika. Na wakati maafa yalishambulia Afrika, Marekani imesaidia kuokoa maisha. Kwa kweli, tulitoa misaada ya kibinadamu zaidi katika Afrika katika kipindi cha miaka minne iliyopita kuliko nchi nyingine yoyote. Kote Sahel, Marekani iliwasilisha misaada ya dharura kwa watu wengi zaidi ya milioni 18 walioathirika katika eneo. Na tulitoa chakula, malazi, na huduma za afya kwa watu karibu milioni tano katika Pembe mwaka jana wakati wa kilele cha ukame.

Tuligundua pia njia ya ubunifu ya kuinua upanuzi wa haraka wa teknolojia ya simu na mtandao. Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ilifadhili "Apps 4 Africa" (Programu kwa Afrika) ushindani ni mfano mmoja. Ushindani huu unahimiza uundaji wa programu za simu za kukuza uchumi, maendeleo, na fursa. Mshindi wa hivi karibuni wa shindano hili ilikuwa programu kutoka Kenya inayoitwa "I-Cow," (I-Ng'ombe) ambayo husaidia wakulima nchini Kenya kusimamia vizuri uzalishaji wa mifugo yao ya ng'ombe.

Ili kukuza fursa kupitia uthabiti na ukuaji wa uchumi, Utawala huupia umeshirikiana na mashirika muhimu ya kieneo. Tulipanua kwa kiasi kikubwa ukubwa wa utume wetu katika Umoja wa Afrika. Waziri Clinton amekuwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa kwanza kuzungumza katika Umoja wa Afrika mnamo Agosti 2011, na alipokea Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika mjini Washington miaka mitatu iliyopita mfululizo. Na Marekani ilijiunga tena na Tume ya Uchumi ya Umoja wa Kimataifa kuhusu Afrika miaka miwili iliyopita ili kuongeza ushiriki wetu katika masuala ya uchumi ya Afrika.

Na wakati tulishirikiana na Afrika katika maeneo haya manne, pia tulilenga kuinua Afrika katika sera yetu ya nje na katika maamuzi ya kimataifa. Kama Waziri Clinton alivyosema mjini Cape Town mwaka jana, "Baadhi ya matatizo yetu ya kimataifa yanahitaji ufumbuzi wa Afrika." Hii ndiyo sababu tumefanya kazi na nchi za Afrika katika masuala kuanzia kwa mabadiliko ya hewa hadi mgogoro nchini Siria.

Hata hivyo, licha ya umbali ambapo Afrika imefikia, na matumaini tuliyo nayo kuhusu mustakabali wa Afrika, bila shaka bado kuna changamoto kubwa. Hebu ningependa kutaja baadhi yake leo.

Wakati Somalia na Sudan ya Kusini zimepata maendeleo makubwa, bado zina mambo mengi ya kufanya. Mali na mashariki mwa DRC zinasababisha vitisho vikubwa kwa utulivu wa kieneo na hatima mamilioni ya raia katika maeneo yaliyoathiriwa na migogoro. Katika Kenya, Marekani tayari imetoa zaidi ya dola milioni 30 tangu 2008 kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi na mipango ya elimu ya wapiga kura, na tutaendelea kushirikiana na Wakenya katika ngazi za juu za serikali yetu ili kusisitiza haja ya uchaguzi wa amani na wa kuaminika mwezi huu wa Machi. Nchini Zimbabwe, tupo imara kuhakikisha kua kura za maoni ya katiba zitakua huru na wazi , itakayofuatiwa na uchaguzi wa kitaifa. Lazima pia tuendelee kutafuta njia za ubunifu zaidi za kukuza biashara na uwekezaji, kukuza fursa, na kuendeleza maendeleo katika Afrika. Na katika kusaidia kushughulikia changamoto zote hizi, lazima tuendelee kuleta usawa kati ya kufikia malengo yetu ya kidiplomasia, na kuwalinda watu wetu iwezekanavyo.

Nilianza hotuba hii kwa kubainisha kwamba nina matumaini makubwa kuhusu Afrika. Mwezi Mei 2000, The Economist lilitoa jalada jeusi pamoja na ramani ya Afrika na picha ya mtoto akiwa ameshikilia roketi ya chini ya kichwa cha habari: "Bara lisilo na matumaini. "Basi, katika Desemba 2011, gazeti lile lile lilichapisha jadala tofauti, wakati huu kukiwa na mtoto aliyekuwa akirusha tiara iliyokuwa na umbo la Afrika chini ya anga ya samawatina kichwa cha habari: "Afrika Inainuka." Hakuna shaka katika akili yangu kwamba Afrika inainuka. Afrika inasonga mbele. Biashara za Marekani, viongozi waliochaguliwa, na MASHIRIKA YASIYO YA SERIKALI (NGOs), nisije nikasahau, wanadiplomasia wa Marekani ambao wanatambua hili sasa watakuwa na faida kubwa zaidi ya wale ambao bado hawajatambua kwamba karne ya 21 itamilikiwa na Afrika.

Asante. Ninatarajia kujibu maswali yenu.